Uncategorized

AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA LEO TAIFA

admin January 18, 2020 7:02 am

ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa leo ataingia uwanjani kwa tahadhari mbele ya Yanga na hesabu zake ikiwa ni kuzipata pointi tatu muhimu.

Azam FC itamenyana na Yanga leo Januari,18 Uwanja wa Taifa utakaochezwa majira ya saa 1:00 Usiku.

Cioaba ambaye anakumbukumbu ya kuifunga Lipuli kwenye mchezo wake wa hivi karibuni amesema kuwa anatambua ugumu wa kucheza na Yanga ila atapambana kupata pointi tatu.

“Ni timu kubwa ambayo nitacheza nayo ila tumejipanga kupata matokeo chanya na tunahitaji kuzipata pointi tatu muhimu kwennye mchezo wetu,” amesema.

Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 29 imecheza mechi 14 na Yanga ipo nafasi ya nane ina pointi 25 imecheza mechi 13.

YOUNG AIPA MKONO WA KWAHERI UNITED, SASA NI MWANA INTER MILAN USHINDI WA MBAO WAMPA KIBURI SVEN, AZITOLEA MACHO POINTI TATU ZA ALLIANCE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply