Uncategorized

HAWA NDIO MAKIPA KIBOKO YA MEDDIE KAGERE, WALICHOMFANYA SIO POA

admin January 21, 2020 3:08 pm


MEDDIE Kagere, mshambuliajI wa Simba, anateswa na mikono ya mlinda mlango wa KMC, Jonathan Nahimana na Razack Abarola kutokana na kuziokoa kiulaini penalti alizowapigia.

Msimu wa mwaka 2018/19 Kagere alimaliza akiwa na mabao 23 ila kwenye jumla ya mabao hayo alikosa penalti moja aliyopiga mbele ya KMC mchezo wa ligi.
Kwenye mchezo huo licha ya KMC kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1, Jonathan Nahimana aliipangua penalti ya Meddie Kagere na kuibuka shujaa wa mechi hiyo ambapo bao la pili lilifungwa na John Bocco kwa mkwaju mwingine wa penalti.
Msimu huu Kagere akiwa na mabao 11 kwenye ligi amepiga jumla ya penalti tatu na hajakosa hata moja ndani ya ligi ila kwenye kombe la Mapinduzi, Razack Abarola wa Azam FC alipangua penalti yake.
Kwenye mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi visiwani Zanzibar, Kagere alipewa jukumu la kupiga penalti ilipanguliwa na Abarola.
Kagere amesema kuwa mpira sio vita licha ya makipa hao kumtesa bado ni marafiki zake kwani wanampa changamoto ya kupambana kuwa bora.
NENO LA SAMATTA KWA WATANZANIA HILI HAPA, MBAYA KWELI KWENYE NYAVU KAKOLANYA ALAMBA SHAVU SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply