Uncategorized

MBELGIJI WA YANGA AWAPA KAZI NYINGINE WACHEZAJI WAKE

admin January 25, 2020 11:26 am


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa washambuliaji wake wote wana kazi moja tu uwanjani kufunga na kutengeneza nafasi za mabao ili kuongeza nguvu ya ushindi kwa timu yake.

Kwenye jumla ya mechi tatu ambazo ameziongoza, Eymael amefunga mabao matatu na kufungwa jumla ya mabao manne jambo ambalo limemfanya alitafutie dawa haraka kabla ya kuivaa Tanzania Prisons kesho kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

“Washambuliaji wangu wote wana kazi moja tu ndani ya Uwanja kutafuta nafasi za kufunga na kuwatengenezea wengine nafasi za kufunga, kitu kikubwa tunachohitaji ni ushindi hakuna jambo jingine. na inawezekana kwa kuwa makosa yaliyopita tumeyafanyia kazi,” amesema.

Miongoni mwa washambuliaji wa Yanga ni pamoja na Ditram Nchimbi, David Mlinga, Patrick Sibomana.

MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED WANA JAMBO LAO FEBRUARI MOSI NYOTA WA KMC AFICHUA KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO YA KUTEMBEZA MABAO 5-0 MBELE YA PAN AFRICAN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply