Uncategorized

YANGA WAJANJA SANA, WAIPIGA BAO MAZIMA SIMBA KWA KIUNGO WAO MPYA

admin January 26, 2020 10:43 am

BERNARD Morrison, kiungo mpya wa Yanga amesema kuwa mashabiki wasiwe na hofu naye ataongeza mkataba mwingine mrefu ili kuendelea kuwapa burudani.

Inaelezwa kuwa, Morrison alipewa kandarasi ya miezi sita inayotoa nafasi kwa wapinzani watani wa jadi wao Simba kufanya mazungumzo naye endapo watamhitaji.

 Kiungo huyo raia wa Ghana amesema hawezi kuwaangusha mashabiki na uongozi wa Yanga kuhusu suala la mkataba wake.

“Nimesaini ndani ya Yana na tayari nimeanza kuzoeana na wachezaji hivyo suala la kusepa kwa sasa halipo na nitazungumza na uongozi ili kujua tunafikia hatua gani hatuwezi kushindwana,”.

Imeelezwa kuwa tayari uongozi wa Yanga umefanya naye mazungumzo kwa ajili ya kumpa mkataba mrefu utakaomzuia kufanya mazungumzo na timu nyingine.


MBWANA SAMATTA AKUTANA NA HILI KUTOKA KWA BOSI WAKE MPYA, KAZI ANAYO MBELGIJI WA SIMBA AWAVAA WACHEZAJI WAKE TENA, KUMBE LUGHA TATIZO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply