Uncategorized

KOCHA SIMBA AFANYA MAAMUZI MAPYA JUU YA KIKOSI CHAKE

admin January 31, 2020 9:22 pm

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vanderbroeck anatarajia kuivunja safu yake ya ulinzi inayoundwa na Muivory Coast, Pascal Wawa pamoja na Erasto Nyoni, kisha kuisuka upya.

Vanderbroeck amefikia hatua hiyo kutokana na kutoridhishwa na uwezo wa mabeki hao katika siku za hivi karibuni na zaidi walipocheza dhidi ya Namungo FC, juzi Jumatano. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar, Simba ilishinda 3-2.

“Kuna makosa mengi ya kiufundi ambayo yamekuwa yakifanywa na safu yangu ya ulinzi kwa upande wa mabeki wa kati na kujikuta tukifungwa mabao ambayo unaweza kuyaita kuwa ni mepesi.

“Nitafanya mabadiliko na kuna uwezekano katika mechi yetu ijayo dhidi ya Costal Union nikawapana nafasi mabeki wengine,” alisema Vandenbroeck na kuongeza kuwa.

“Katika mechi nne tulizocheza hivi karibuni, licha ya kushinda lakini tumekuwa tukiruhusu mabao.”

Matokeo ya mechi hizo ni: Mbao 1-2 Simba, Alliance 1-4 Simba, Simba 2-1 Mwadui na Simba 3-2 Namungo.
MANE WA LIVERPOOL AIBUKIA YANGA KWA MTINDO HUU KIPA YANGA ATIMKIA KENYA, UONGOZI WAFAFANUA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply