Uncategorized

MTIBWA SUGAR: LIGI YA MSIMU HUU NI BALAA

admin February 4, 2020 9:09 am

ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa ushindani wa msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara ni mkubwa jambo ambalo linafanya kila timu kupambana kutafuta matokeo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila amesema kuwa kila timu nyingi zinaishi kwenye malengo ambayo zimejiwekea jambo linalofanya ligi izidi kuwa nzuri.

“Ligi kiujumla kwa sasa imechangamka kila timu inaonyesha kile ambacho inastahili kukipata ndani ya uwanja. Timu nyingi zimegunuda siri ya kupata matokeo ni kujituma jambo hili linafanya ligi izidi kukua.

“Kwa upande wetu nasi pia tupo vizuri licha ya kupoteza mbele ya Yanga haina maana kwamba tumeshindwa. Matokeo ya mpira yanatupa mwanga wa kufanya kitu kingine,” amesema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 imecheza jumla ya mechi 18 na imejikusanyia pointi 23 kibindoni.

SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA POLISI TANZANIA LEO, TAIFA MZUNGU WA YANGA: TARATIBU WACHEZAJI WANAKUJA, WATAFANYA MAKUBWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply