Uncategorized

SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA POLISI TANZANIA LEO, TAIFA

admin February 4, 2020 8:09 am

SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kuzisaka pointi tatu leo mbele ya Polisi Tanzania.

Simba itamenyana na Polisi Tanzania, Uwanja wa Taifa saa 1:00 Usiku kwenye mchezo wao wa kwanza msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara.

Sven amesema kuwa makosa waliyoyafanya kwenye mchezo wao uliopita mbele ya Coastal Union wameyafanyia kazi jambo litakalowapa nguvu ya kuendelea kupambana.

Kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini amesema kuwa anatambua ushindani ni mkubwa na anacheza na mabingwa watetezi hilo halimpi shida anawaamini wachezaji wake.

Timu zote mbili zimecheza jumla ya mechi 18 na leo zinakamilisha mzunguko wa kwanza rasmi kabla ya kuanza kufukuzia kete za mzunguko wa pili.

Simba mchezo wake uliopita ilishinda mabao 2-0 mbele ya Coastal Union ya Tanga huku Polisi Tanzania ikishinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania.

AZAM FC SI YA MCHEZO, ILICHOFANYA JANUARI NI SHIDA TUPU MTIBWA SUGAR: LIGI YA MSIMU HUU NI BALAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply