Uncategorized

MATAMKO YA KOCHA YANGA JUU YA NIYONZIMA

admin February 7, 2020 9:14 pm

Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa miongoni mwa vitu anavyojivunia ndani ya Yanga ni kuwa na aina ya wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na Haruna Niyonzima na Mapinduzi Balama.

Luc alisema kuwa amemtazama Niyonzima kwenye mechi zake zote alizoanza sio mwepesi wa kupoteza mipira anayopewa pamoja na uwezo wake wa kutuliza wachezaji wakiwa wamekasirika.

β€œMchezaji mzuri unamtambua siku utakayomuona uwanjani kwa namna anavyofanya kazi yake kwa juhudi bila kuchoka na kuwa msaada kwa wengine na sio mzigo, ndivyo ilivyo kwa Niyonzima.

β€œJaribu kumtazama kabla hajapewa mpira anatoa maelekezo, akiwa na mpira anatoa maelekezo kupitia viungo vyake, ni aina ya wachezaji ambao wanatakiwa kwenye timu inayotafuta ushindi, hawatofautiani na (Balama) Mapinduzi  ambaye anajipa kazi ile aliyotumwa ndani ya uwanja,” alisema Luc.
JEMBE JIPYA YANGA LAREJEA SIMBA : WAPINZANI WETU WALIKUWA VIZURI, TULISHINDWA KUTUMIA NAFASI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply