Uncategorized

HAO AZAM FC WAIPANIA POLISI TANZANIA KESHO UHURU

admin February 10, 2020 2:27 pm


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kesho utapambana kuzipata pointi tatu za Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.

Azam ina kumbukumbu ya kushinda mabao 3-1 mbele ya KMC kwenye mchezo wa ligi kuu, tayari wameanza mazoezi kuiwinda Polisi Tanzania.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa baada ya kuichapa KMC walianza kuiwinda Polisi Tanzania.

“Niseme kwamba kikosi kipo vizuri na wachezaji wana morali ya kutosha kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Polisi Tanzania.

“Ushindi wetu mbele ya KMC unatupa nguvu ya kupambana na kuendelea kusaka matokeo zaidi kikubwa ni sapoti kwa mashabiki ili kuona timu ikitoa burudani,” amesema.

MBELGIJI WA SIMBA ATOA KAULI YA KISHUJAA, WAAMUZI WATAJWA HUYO RONALDO NI NOMA NDANI YA SERIA A CHEKI ALICHOFANYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply