Uncategorized
AZAM WATINGA KWA MKUU WA MKOA WA LINDI
Timu ya Azam FC leo Februari 19, imekwenda kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mh. Godfrey Zambi.
Msafara wa Azam FC kwenda kwa Zambi, uliongozwa na Meneja Masoko wa timu hiyo, Tunga Ally, Kocha Msaidizi, Idd Nassor Cheche na Ofisa Habari, Jaffar Idd.
Azam FC ina kibarua cha kumenyana na Ndanda FC ya Mtwara mchezo utakaochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.