Zubery Katwila Geita Gold
Michezo Bongo

Katwila Aainisha Mipango Geita Gold: “Bukombe Kitakuwa Mwiba”

Vardo August 30, 2026 7:55 am

BAADA ya kuvuna pointi nne muhimu katika mechi mbili mtawalia za nyumbani, Kocha Mkuu wa Geita Gold, Zubery Katwila, ametuma ujumbe mzito kwa timu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara akisisitiza kuwa Uwanja wa Bukombe utakuwa ngome isiyopitika kirahisi msimu hii.

Geita Gold, ambayo imerejea Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026 baada ya kushuka daraja msimu wa 2023-2024, imeonyesha ukomavu wa hali ya juu ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani uliopo mji mdogo wa Ushirombo, Wilayani Bukombe, Mkoani Geita.

Katika mechi hizo za nyumbani, Geita Gold ilianza kwa kuisambaratisha Kagera Sugar kwa mabao 6-2 mnamo Agosti 22, 2026, kabla ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya miamba Azam FC mnamo Agosti 28, 2026.

Katwila Afunguka Mkakati Wake

Akizungumza kuhusu mwenendo wa timu yake, Katwila alieleza kuwa matokeo hayo yamejenga hali ya kujiamini kikosini na kuongeza morali ya wachezaji kuelekea mechi zijazo.

“Ushindani wa ligi ni mkubwa sana. Mechi yetu dhidi ya Azam FC ilikuwa ngumu na kuamini kwamba tutasawazisha na kuondoka na pointi moja inathibitisha ukomavu tulionao. Matokeo haya yametupa nguvu ya kuhakikisha uwanja wetu wa nyumbani unakuwa sio rafiki kwa timu yoyote inayokuja kucheza hapa Bukombe,” alisema Katwila.

Kocha huyo alitumia fursa hiyo kuwapongeza wachezaji wake kwa nidhamu na uwezo mkubwa wa kupambana uwanjani, huku akiwataka kuendelea na moto huo huo ili kuwapa furaha mashabiki wa Mkoa wa Geita na Ukanda mzima wa Ziwa.

Mwenendo wa Geita Gold Ligi Kuu (Mechi 4 za Kwanza):

  • Mbeya City 0-1 Geita Gold (Agosti 14, 2026) – Ushindi

  • Namungo FC 1-0 Geita Gold (Agosti 18, 2026) – Kipigo

  • Geita Gold 6-2 Kagera Sugar (Agosti 22, 2026) – Ushindi

  • Geita Gold 2-2 Azam FC (Agosti 28, 2026) – Sare

Oscar Mwajanga Aweka Wazi Vita ya Mabao Mbeya City, Acha Ujumbe Mzito Farid Mussa Aivaa Coastal Union: “Uzoefu Wangu Utatubeba Ligi Kuu”