Cheikh Toure Yanga
Yanga SC

Dabo Aibuka na Kumjuza Mbinu Toure ya Kutoboa Yanga na Ligi Kuu

Vardo August 30, 2026 7:46 am

KOCHA wa zamani wa Azam FC, Yusuf Dabo, ameibuka na kumtumia ujumbe mzito mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Cheikh Toure, huku akimpa mbinu za kiufundi zitakazomsaidia kutoboa na kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Toure (29), raia wa Senegal mwenye uraia wa Ufaransa, alijiunga na Yanga mwezi Julai 2026 kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Al-Jabalain FC ya Saudi Arabia—ambako alikuwa na msimu bora uliopita akifunga mabao 19 na kutoa asisti 5 katika mechi 34.

Akizungumzia ubora wa nyota huyo anayevaa jezi namba tisa ndani ya Wananchi, Dabo alisema Toure ana uwezo mkubwa wa kufunga, lakini lazima ajiandae kimwili na kisaikolojia ili kuhimili mikiki mikiki ya mabeki wa Ligi Kuu Bara.

“Namfahamu vizuri Toure na najua uwezo wake, lakini anatakiwa kujiandaa sana kiushindani kwa sababu Ligi ya Tanzania si rahisi. Hapa unahitaji kuwa tayari kupambana kwa nguvu na kutumia uwezo wako kwenye mazingira yenye ushindani mkubwa,” alisema Dabo.

Dabo aliongeza kuwa soka la Bongo linahitaji matumizi makubwa ya nguvu, na akatoa mfano wa washambuliaji waliowahi kutua Azam FC kutoka Amerika ambao walishindwa kufanya vizuri kutokana na kushindwa kuendana na aina hiyo ya uchezaji.

Pia, alisisitiza kuwa Yanga ni timu yenye shinikizo kubwa la matokeo kutoka kwa mashabiki, lakini ana imani Toure akianza kucheka na nyavu tu, kila kitu kitakaa sawa na mashabiki watamwelewa.

Hadi sasa, Toure ameshafunga bao moja na kutoa asisti moja, huku akiwa amecheza mechi za ligi dhidi ya Namungo, Coastal Union, na JKT Tanzania.

Manqoba Mngqithi Anena Zito Hali ya Aziz Ki Yanga SC Oscar Mwajanga Aweka Wazi Vita ya Mabao Mbeya City, Acha Ujumbe Mzito