OLE Gunnar Solskajer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa atamuongezea msimu mmoja Odion Ighalo raia wa Nigeria iwapo ataonyesha ubora.
Nyota huyo amesajiliwa na United kwa mkopo akitokea Klabu ya Shangai Shenhua ya China.
“Iwapo ataonyesha ubora na kufanya kazi yake kwa umakini anaweza kukaa zaidi ndani ya Old Traford.
“Ni mkopo kweli ninajua ila unapokuwa mlangoni na kuonyesha juhudi inatoa nafasi kwako kupewa muda zaidi ndani ya kikosi ndivyo itakavyokuwa kwake pia,” amesema.







