Uncategorized

MTIBWA SUGAR WAIBUKIA HUKU BAADA YA POINTI MOJA

admin February 20, 2020 8:22 am


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kilichoifanya timu yake kushindwa kupata matokeo mbele ya Tanzania Prisons ni ubovu wa Uwanja wa jamhuri ambao waliutumia.

Mtibwa Sugar iliambulia pointi moja mbele ya Tanzania Prisons na walipata pigo la kumkosa kiungo wao Abdulhalim Humud ambaye alionyeshwa kadi nyekudu.

“Nashukuru kupata pointi moja ugenini, haikwuwa malengo yetu na tumeshindwa kutokana na mazingira ya uwanja kutokuwa rafiki kwetu kupata matokeo.

“Nawapongeza wachezaji kwa kujituma, makosa ambayo yametokea tutayafanyia kazi ili kurejea kwenye ubora wetu kwenye mechi zinazofuata,” amesema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 24 imecheza mechi 23 za ligi.

AZAM FC: MAPAMBANO BADO YANAENDELEA, AKILI ZETU SASA NAMUNGO COASTAL UNION YAWAOMBA RADHI MASHABIKI, HUYU HAPA CHANZO CHA KUPOTEZA MBELE YA RUVU SHOOTING

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply