Uncategorized

BIASHARA UNITED WAIPIGIA HESABU HIZI SAFU YA USHAMBULIAJI YA SIMBA KESHO TAIFA

admin February 21, 2020 4:22 am


OMARY Madenge, Kocha Msaidizi wa Biashara United amesema kuwa mpango mkubwa kwa timu yake ni kupambana mbele ya Simba na kupata pointi tatu bila kuhofia makali ya washambuliaji wa wapinzani wake.

Biashara United ya Mara, itashuka Uwanja wa Taifa kesho kumalizana na Simba mchezo wa pili ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0.

Madenge amesema:”Tupo tayari kupambana mbele ya safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Meddie Kagere, tunajua uimara wao ulipojificha nasi hatuna mashaka tupo vizuri, mashabiki watupe sapoti,”.

Biashara United ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 32 kibindoni.

COASTAL UNION YATUMA UJUMBE HUU KWA YANGA JEMBE LA KAZI SASA LAANZA MAZOEZI NDANI YA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply