Uncategorized

RUVU SHOOTING YAIPIGA MKWARA POLISI TANZANIA, YATAMBA ISHU YA KUPAPASA INAENDELEA

admin February 22, 2020 1:41 am


RUVU Shooting iliyo nafasi ya 10 na pointi zake 32 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo itakaribishwa na Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika Moshi.


Polisi Tanzania wao wapo nafasi ya nane na kibindoni wana pointi 34 zote zikiwa zimecheza mechi 23.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa malengo makubwa ya timu yake ni kuendeleza falsafa ya kupapasa baada ya kumalizana na Coastal Union.

“Hakuna tunachokihitaji zaidi ya kuendelea falsafa yetu ya kupapasa, tumemalizana na Coastal Union sasa ni zamu ya Polisi Tanzania,” amesema.
MTIBWA SUGAR YAJIPA MATUMAINI KUTUSUA MBELE YA MBEYA CITY LEO KAGERA SUGAR KUPOTEZEA MAUMIVU YA SIMBA KWA WABAYA WA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply