Uncategorized

COASTAL UNION V YANGA WAPIGANA MKWARA HUU

admin February 23, 2020 12:41 pm

JUMA Abdul, beki wa Yanga na nahodha msaidizi wa kikosi hicho amesema kuwa kesho watapambana mbele ya Coastal Union ili kupata ushindi mbele ya wapinzani wao utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Yanga itakaribishwa na Coastal Union iliyotoka kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao 2-1 na Ruvu Shooting huku wao wakitoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa wachezaji wana morali kubwa na wamejipanga kupata matokeo mbele ya wapinzani wao Coastal Union.
“Ligi ina ushindani mkubwa nasi tunapambana kurejea kwenye ubora wetu, matumaini yetu ni kuona tunapata pointi tatu, mashabiki watupe sapoti kwani safu ya ulinzi makosa yetu tumeyafanyia kazi,” amesema Abdul mwenye pasi nne za mabao.
Bakari Mwamnyeto, beki na nahodha mwenye bao moja na asisti moja ndani ya Coastal Union amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kupata ushindi mbele ya wapinzani wao.
JONAS MKUDE HATA WEWE PIA UMO, WACHEZAJI NI MUHIMU KUTUMIA AKILI HAYA MABAVU HAYAFAI KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA COASTAL UNION, MKWAKWANI TANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply