Uncategorized

NYOTA HAWA WA KIGENI WATANO TU UHAKIKA KIKOSI CHA KWANZA YANGA

admin February 23, 2020 4:41 am


PAPY Tshishimbi nahodha wa Yanga amepewa jukumu la kuwaongoza wachezaji wenzake wageni pamoja na kikosi cha Yanga kwenye mechi zote za mikoani ambazo timu yake itacheza.

Imeelezwa kuwa wachezaji wengine wageni ambao watafanya kazi kwa ukaribu na Tshishimbi ni pamoja na Haruna Niyonzima, Lamine Moro na Bernard Morisson kutokana na kuonyesha kiwango kilichokubalika ndani ya benchi la ufundi linaloongozwa na Luc Eymael.

Wachezaji hao wote ambao ni wageni imeelezwa kuwa wamepitishwa na Kocha Mkuu Eyamel kucheza kwenye viwanja vya mikoani kutokana na kumudu ushindani wa ugumu wa viwanja vya mkoani.


 “Benchi la ufundi limekubaliana baada ya kufanya tathimini kwenye mechi dhidi ya Polisi Tanzania na kupata wachezaji wanaoumudu viwanja vya nje ya Dar.

 “Kikubwa walichokubaliana ni kuwatumia wachezaji wazawa ili kuwapa nafasi kutumia uzoefu kwenye viwanja vya nyumbani walivyovizoea,”. Imeeleza taarifa hiyo.

Yanga leo ina kibarua cha kutafuta pointi tatu mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kikubwa ambacho wanakifanya kwa sasa ni kujenga timu yenye ushindani itakayopata matokeo kwenye mechi zake zinazofuata.

TWIGA STARS YASHIKA NAFASI YA TATU MASHINDANO YA UNAF SIMBA BAADA YA KUMALIZIANA NA BIASHARA SASA HAO KWA STAND UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply