Uncategorized

YANGA YAFUTA BUNDI LA SARE, LAICHAPA ALLIANCE MABAO 2-0 UWANJA WA TAIFA

admin February 29, 2020 7:48 pm


TIMU ya Yanga leo imefuta bundi la sare iliyokuwa ikiwaandama kwa kushinda mbele ya Alliance FC mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Februari 29 Uwanja wa Taifa.

Ushindi huo uewafanya mashabiki kujawa na furaha na kusahau sare nne mfululizo kwa mwez Februari mbele ya Mbeya City, Prisons, Polisi Tanzania na Coastal Union.

Mabao yote ya Yanga yamepachikwa kimiani na nyota wao mpya aliyejiunga na timu hiyo akitokea Polisi Tanzania alikokuwa kwa mkopo akitokea Azam FC, Ditram Nchimbi.

Allingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Tariq Seif dakika ya 45 na alifunga mabao hayo dakika ya 48 kwa kichwa akimalizia pasi ya Bernard Morrison na dakika ya 78 baada ya mabeki wa Alliance kujichanganya.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuongeza pointi tatu ila inabaki nafasi ya nne ikiwa na pointi 44.

KOSA KUBWA LA MTIBWA SUGAR KUMBE ILIKUWA KUZITUNGUA SIMBA NA YANGA WATFORD SIO WATU WAZURI, WATIBUA REKODI ZA LIVERPOOL KIBABE, YAICHAPA 3-0

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply