Uncategorized

YANGA YATAJA MBINU ZITAKAZOWAPA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

admin March 2, 2020 7:19 am


KESHO Yanga itakuwa na kazi ya kusaka ponti tatu mbele ya Mbao FC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa1:00 usiku.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa wanachohitaji ni mwendelezo wa ushindi kwenye ligi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa amekuwa akikitazama kikosi chake kwa muda mrefu na kukifanyia marekebisho pale kinapokwama ili kuwa bora.

“Nimekuwa nikifanya kazi kwa ukaribu na wachezaji wangu na kuona namna gani tunakuwa bora, tuna mechi nyingi ambazo zinatukabili na zote ngumu tunachokifanya ni kuona namna gani tutapata matokeo.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwani uwezekano wa kupata matokeo upo na uwezo upo mikononi mwa wachezaji,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya nne ikiwa imecheza mechi 23 ina pointi 44 kibindoni.

SHIME AWAPA TANO WACHEZAJI KUICHAPA UGANDA, MASHABIKI WAHUSIKA MUDA WA KUJIPANGA KWA TIMU ZILIZOBORONGA MZUNGUKO WA KWANZA BADO UPO KIKUBWA KUJITUMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply