Uncategorized

SHIME AWAPA TANO WACHEZAJI KUICHAPA UGANDA, MASHABIKI WAHUSIKA

admin March 2, 2020 6:19 am


KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 amesema kuwa siri kubwa ya ushindi ni sapoti ya mashabiki kujitokeza Uwanja wa Taifa pamoja na juhudi za wachezaji ndani ya uwanja.


Jana, Machi Mosi, timu ya Wanawake ya U 17 ilishinda kwa mabao 2-1 mbele ya Uganda mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.

Uganda ilianza kuliandama lango la Tanzania dakika ya sita kupitia kwa Fauzia Najeba na kuamsha hasira za Tanzania kupitia kwa Aisha Masaka dakika ya 28 na 87.

Ushindi huo unaiweka kwenye nafasi Tanzania kufuzu Kombe la Dunia kwa Wanawake linalotarajiwa kufanyika India.

“Kikubwa wachezaji walitambua kwamba wapo nyumbani na mashabiki wamejitokeza kuwapa sapoti wamejituma na wamepata matokeo mazuri, tunajipanga ili kuona tunafikia malengo ya kushiriki Kombe la Dunia,” amesema.
AZAM FC KUANZA KULISHUGHULIKIA TATIZO HILI MAPEMA NDANI YA TIMU YAO YANGA YATAJA MBINU ZITAKAZOWAPA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply