Timu zenye mashambulizi makali Ulaya
Habari za michezo

Maajabu Ya Orodha Ya Timu 10 Zenye Mashambulizi Makali Ulaya: Real Madrid Yaangukia Pua, Brighton Yaweka Rekodi

Vardo October 2, 2026 5:19 pm

ZURICH, USWISI — Mtandao mashuhuri wa takwimu za soka wa Transfermarkt umetaja orodha ya timu 20 zenye safu hatari zaidi za ushambuliaji barani Ulaya msimu huu. Hata hivyo, matokeo ya takwimu hizo yameleta mshangao mkubwa baada ya miamba kama Real Madrid kukwama nafasi ya tisa, huku Brighton ya Ligi Kuu England (EPL) ikishika namba tatu kwa kishindo.

Vipimo hivyo vimetokana na wastani wa mabao kwa kila mchezo (GPG – Goals Per Game) katika ligi kuu tano bora za Ulaya: Premier League, LaLiga, Serie A, Bundesliga, na Ligue 1.

Katika mchanganuo huo, Bundesliga ya Ujerumani imetawala kwa kutoa timu saba kwenye 20 bora, huku Ligue 1 ya Ufaransa ikiwa na timu mbili pekee.

Hii Hapa Orodha Ya Timu 10 Bora Zenye Mashambulizi Hatari Ulaya:

1. FC Barcelona (LaLiga) – 4.43 GPG

Miamba wa Hispania chini ya kocha mpya Hansi Flick ndio kinara wa Ulaya. Wakiwa wameshinda mechi zote saba za kwanza za LaLiga, Barca imepachika mabao 31. Mshambuliaji Raphinha amekuwa mwiba mchungu akihusika moja kwa moja kwenye mabao 12.

2. Bayern Munich (Bundesliga) – 3.50 GPG

Mabingwa hao wa zamani wa Ujerumani wanashika nafasi ya pili wakiwa na wastani wa mabao 3.50 kwa mchezo katika mechi zao nne za kwanza za Bundesliga.

3. Brighton & Hove Albion (EPL) – 3.20 GPG

Ndio mshangao mkubwa zaidi msimu huu! Brighton imepanda hadi nafasi ya tatu baada ya kufunga mabao 16 katika mechi zake tano za kwanza—idadi kubwa zaidi kuliko hata vinara wa EPL, Manchester City waliotupia mabao 13.

4. SC Freiburg (Bundesliga) – 3.00 GPG

Freiburg imeingia tano bora baada ya kupachika mabao 12 katika michezo nne pekee ya Bundesliga.

5. Inter Milan (Serie A) – 3.00 GPG

Miamba hawa wa Italia wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Serie A, wameingia kambani mara 15 katika mechi tano za kwanza.

6. AS Roma (Serie A) – 2.80 GPG

Roma inakamata nafasi ya sita ikiwa imetupia mabao 14 katika michezo mitano.

7. FC Augsburg (Bundesliga) – 2.75 GPG

Wajerumani hawa wamefunga mabao 11 katika mechi nne pekee za kwanza za ligi kuu.

8. Manchester City (EPL) – 2.60 GPG

Vinara hawa wa Uingereza wanashika nafasi ya nane wakiwa wamefunga mabao 13 hadi sasa.

9. Real Madrid (LaLiga) – 2.57 GPG

Licha ya kuwa na safu iliyosheheni nyota wakubwa duniani, Miamba hawa wa Madrid wanashika nafasi ya tisa wakiwa wamefunga mabao 18 katika mechi saba.

10. Bayer Leverkusen (Bundesliga) – 2.50 GPG

Mabingwa watetezi wa Ujerumani wanakamilisha 10 bora wakiwa wameingia kambani mara 10 katika mechi nne.

Mbio Mpya Ya Paka Na Panya Yafika Meridianbet Pacome Zouzoua Aweka Magongo Chini Yanga SC: Aanza Mchakato wa Tiba Nje ya Nchi