Mechi za Leo UEFA Nations League na AFCON
Meridianbet

Viwanja Mbalimbali Kuwaka Moto Siku ya Leo

Vardo November 17, 2026 1:52 pm

Mataifa Mbalimbali kushuka Dimbani kusaka pointi 3 za ushindi. Huku AFCON kule Uefa Nations League. Je nani kuondoka nyumbani na ushindi?

Moto utawaka kwenye mechi ya Denmark dhidi ya Norway ambapo kwenye msimamo wa Kundi wanapishana pointi 3 pekee, hii ni mechi ambayo kila timu inahitaji ushindi ili kuweza kujiweka kwenye nafasi ya pili.

Denmark ametoka kushinda mechi yake iliyopita hivyo anaingia kwenye mchezo huu akiwa na ari ya nguvu kabisa, halikadhalika kwa Norway naye amtoka kutoa dozi kubwa.

Timu zote zina wachezaji wakubwa na ambao wanacheza ligi kubwa wakiwemo kina Haaland, Hojlund, Odergaard na wengine wengi.

Mechi nyingine ya UEFA NATIONS ni hii inayowakutanisha kati ya Wales dhidi ya Ureno moja ya mechi ambayo itakuwa ikitazamwa sana kutoka na matokeo yao yaliyopita, ambapo timu hizi zote zimetoka kupoteza michezo yao iliyopita.

Lakini kwa upande wa Ureno hali imekuwa mbaya zaidi baada ya kupokea kipigo kizito kabisa huku maneno yakiibuka kwamba kutokuwepo kwa Ronaldo pia imechangia hivyo timu hiyo chini ya kocha mkuu Jorge inabidi ijiangalie.

Mechi hizi unaweza ukazipata kule Meridianbet, lakini pia bila kusahau msimamo wa makundi mbalimbali, taarifa za wachezaji majeruhi na wachezaji wanaoongoza kwa ufungaji magoli.

Vijana wa Bellamy, Wales wanahitaji matokeo mazuri katika mchezo huu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuepuka kushuka daraja, lakini wanakutana na Ureno yenye kikosi chenye uzoefu na ubora mkubwa.

Wales imekuwa na wakati mgumu katika michezo ya hivi karibuni, ikipoteza mechi nne kati ya tano za Nations League. Hata hivyo, uwepo wa Harry Wilson, David Brooks na Brennan Johnson unaweza kuongeza makali katika safu yao ya ushambuliaji.

Kwa upande wa Ureno, licha ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Denmark katika mchezo uliopita, wana wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha matokeo kama Bruno Fernandes, João Félix na Gonçalo Ramos. Pia, Ureno itahitaji kujipanga upya katika safu ya ulinzi kutokana na kukosekana kwa Rúben Dias, huku Wales ikitafuta kutumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo mazuri.

Lakini pia ile michuano ya kufuzu AFCON inaendelea kwa michezo mingi lakini sisi tutajikta na mchezo wa Tanzania dhidi ya Nigeria huku hii ikiwa ni mechi ya kisasi kwa wenyeji baada ya kupigika kwenye mechi ya kwanza walipokutana.

Kwenye Kundi lao, Tanzania ambao ni moja ya wenyeji wa michuano hii 2027, wapo nafasi ya mwisho ambayo ni ya mwisho, huku Nigeria wao wakiwa nafasi ya 2 kwenye msimamo baada ya kujikusanyia pointi zao 6.

Chini ya kocha mkuu Gamondi bado Stars haipewi nafasi ya kushinda mechi hii kutokana na ubora wa wachezaji ambao timu pinzani inayo, pia wengi wa wachezaji wao wanacheza kwenye ligi kubwa Duniani. Je hii ni mechi ya wenyeji kushinda?.

Habibu Kinyogoli Afariki Dunia: Pigo Kubwa Mchezo wa Ngumi Tanzania Burudani ya Krismasi Yawasili Meridianbet!