Uncategorized

POLISI TANZANIA: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA MWADUI

admin March 4, 2020 7:49 am


MARCEL Kaheza mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa leo watakuwa na kazi kubwa ya kuzisaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Kambarage.

Kaheza amekuwa kwenye ubora wake msimu huu chini ya Malale Hamsini ambaye ni Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amehusika kwenye mabao tisa kati ya 27 waliyofunga Polisi Tanzania akifunga mabao matano na pasi nne za mabao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa wamekuwa wakipewa mbinu nyingi zinazowafanya wawe bora jambo analoamini litawapa matokeo chanya kwa wapinzani wao.
β€œKocha amekuwa akitupa mbinu nyingi na nzuri ambazo zinaeleweka na tunazifuata tukiwa uwanjani kutafuta matokeo tuna amini kwamba tutapata matokeo kwenye mechi zetu zote tunazocheza tunahitaji pointi tatu,” amesema Kaheza.
NAMUNGO YAIPIGA MKWARA MTIBWA SUGAR SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KWA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply