Uncategorized

GEITA GOLD WAPANIA KUSHIRIKI LIGI KUU BARA

admin March 6, 2020 12:05 pm

UONGOZI wa Geita Gold, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza umesema kuwa mipango yao ni kuona wanatimiza malengo yao ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao kwa kupambana kwenye mechi zao wanazocheza.

Geita Gold ipo Kundi B ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 16 na ina pointi 26, kinara wao wa kucheka na nyavu ni George Mpole ambaye amefunga mabao nane na katika mabao hayo ana hat trick moja aliyofunga mbele ya Pamba Sports Club mchezo uliochezwa Uwanja wa Nyankumbu Sekondari.

Ofisa Habari wa Geita Gold, Gabriel Nyasilu, maarufu kama Gabo amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wachezaji wanapambana kuona wanafikia malengo waliyojiwekea.

“Ni kazi kubwa na ushindani upo ila tunahitaji kuona malengo yetu ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao yanatimia, mashabiki watupe sapoti,” amesema,
KOCHA AMBEBESHA ZIGO LA LAWAMA KIPA LIPULI, KISA KUFUNGWA MABAO MATATU JOKATE AWAITA MASHABIKI WA YANGA TAIFA WAKAIMALIZE SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply