Uncategorized

RAIS CAF KUTUA BONGO KUISHUHUDIA YANGA NA SIMBA LIVE

admin March 6, 2020 10:05 am


AHMAD Ahmad, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba utakaochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa, Jumapili.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 11:00 umekuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wote kiujumla.

Ahmad anatarajiwa kutua nchini Tanzania kesho ikiwa ni maalumu kwa ajili ya ziara ya siku tatu nchini.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Clifford Ndimbo amesema kuwa maandalizi ya kumpokea Ahmad yamekamilika.

“Kila kitu kipo sawa na tunatarajia kumpokea Rais wa Caf ambaye atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Yanga na Simba kwa kuwa aliomba kwa Rais wa TFF, Wallace Karia kuja kuishuhudia mechi hiyo,”.

HESABU ZA MTIBWA SUGAR ZIPO NAMNA HII AZAM FC V ALLIANCE NI VITA YA KISASI KESHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply