KIKOSI cha Yanga leo kimekubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya KMC mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Kichapo cha leo ni cha nne kwa Yanga iliyocheza mechi 26 ikiwa na pointi 50 kibindoni inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Bao pekee la ushindi lilifungwa na Salim Aiyee dakika ya 62 kwa shuti lililomshinda mlinda mlango Metacha Mnata.
Ushindi huo unaifanya KMC kusepa na pointi tatu jumla za Yanga na kufikisha pointi 30 na kupanda kutoka nafasi ya 18 mpaka 16 kwenye msimamo.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.