Uncategorized

SABABU YA AJIBU, KICHUYA, KAKOLANYA KUSOTA BENCHI HII HAPA, MZUNGU AWAPA MASHARTI MAZITO

admin March 13, 2020 9:54 pm

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wote ni wazuri ila anashindwa kuwatumia kutokana na kushindwa kumshawishi pale wanapopata nafasi.


Miongoni mwa nyota ambao wamekuwa wakikosekana uwanjani ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Yusup Mlipili,Beno Kakolanya.

Kichuya, Kakolanya na Ajibu mchezo wao wa mwisho ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Stand United huku Mlipili akiwa nje kwa muda mrefu.

Sven amesema kuwa wachezaji ambao hawatumii bado hawajamshawishi jambo ambalo linamfanya asiwatumie na kutaka wakipata nafasi wafanye kazi kubwa kumshawishi ili wapate nafasi.

“Kuna wachezaji wengi na wote ni wazuri hivyo kinachonifanya nisiwatumie wachezaji wengine ni kushindwa kwao kunishawishi, wakipata nafasi wanatakiwa kuonyesha uwezo wao wote,” amesema.
HII NOMA, MUUAJI WA SIMBA AWAPIGA MKWARA WA MAANA WATANI ZAKE NAMUNGO YAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply