Uncategorized

KAMBI YA TIMU YA JKT TANZANIA YAVUNJWA RASMI LEO

admin March 18, 2020 4:42 pm

UONGOZI wa Klabu ya JKT Tanzania, leo Machi 18,2020 rasmi umevunja kambi yake kutokana na maelekezo yaliyotolewa jana na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa kuhusu zuio la kuwepo kwa mikusanyiko mbalimbali kutokana na kuwepo ugonjwa wa Corona hapa nchini.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa JKT Tanzania , Jamila Mutabazi imeeleza kuwa wachezaji wote wanarejea nyumbani kuanzia leo.

Pia wachezaji wametakiwa kuendelea kujikinga na kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali sambamba na wataalam wa afya.

YANGA: TULIWABANA MBAVU NAMUNGO, WASHUKURU MWAMUZI BRUNO APIGA MKWARA MZITO KWAMBA MOTO WAKE BADO SANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply