Uncategorized

YANGA: TULIWABANA MBAVU NAMUNGO, WASHUKURU MWAMUZI

admin March 18, 2020 3:42 pm

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwassa amesema kuwa Namungo FC washukuru bahati haikuwa yao kwani waliwabana mbavu na kushinda bao la halali ambalo lilikataliwa na mwamuzi kwenye mchezo wao uliochezwa Machi 15.2020.

Kwenye mchezo huo Yanga walifanya shambulizi la pili na kufunga bao kupitia kwa Tariq Seif lilikataliwa na mwamuzi kwa kutafsri kwamba mlinda mlango Nurdin Barola alichezewa faulo jambo ambalo liliwanyima ushindi.

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 ambapo Yanga ilianza kufunga kupitia kwa Tariq Seif na la Namungo lilifungwa kupitia kwa Bigirimana Blaise.

“Tuliwabana na wachezaji wetu walicheza kwa umakini, bao letu tulilowafunga kupitia kwa Tariq ambalo lilikataliwa lilikuwa ni la ushindi ila changamoto imekuwa kwa waamuzi,” amesema.

Yanga imecheza mechi 27 imefunga mabao 31 ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 51 kibindoni.

SASA LIGI KUU BARA KUCHEZWA BILA MASHABIKI UWANJANI KAMBI YA TIMU YA JKT TANZANIA YAVUNJWA RASMI LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply