Uncategorized

MBELGIJI WA YANGA AOMBA MUDA KUKIJENGA KIKOSI KIWE BORA ZAIDI

admin March 21, 2020 4:01 pm


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anaamini akipewa muda atakijenga kikosi cha Yanga na kuwa bora zaidi ya sasa.

Kocha huyo amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi 15 za Ligi Kuu Bara ambazo ni sawa na dakika 1,350 ambapo kwenye mechi yake ya kwanza ya dabi alishinda kwa bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kwenye mchezo huo Yanga ilianza kupata bao la ushindi dakika ya 44 kupitia kwa Bernard Morrison aliyefunga kwa adhabu ya faulo akiwa nje ya 18 na kuwafanya wasepe na pointi tatu mbele ya Simba.

Eymael amesema kuwa kila siku anaona kuna mabadiliko ndani ya kikosi chake jambo ambalo linamfanya aamini kwamba watakuja kufanya vizuri wakati ujao.

“Wachezaji wanafanya vizuri na wanapenda kazi yao, nina amini wakati ujao watakuwa bora zaidi ya sasa ni suala la muda tu kwa sasa ili kuona namna gani tutapata matokeo.

“Mashabiki wamekuwa nasi bega kwa bega ni suala la kuwashukuru katika hili waendelee kutupa sapoti hatutawaangusha,” amesema.

MANCHESTER UNITED WAINGIA KWENYE VITA NA BARCELONA,PSG KUISAKA SAINI YA AUBA SABABU YA MBEYA CITY KUWA NAFASI YA 17 HII HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply