Uncategorized

WINGA CHELSEA AIKUMBUKA FAMILIA YAKE

admin March 21, 2020 12:01 pm


NYOTA wa timu ya Chelsea, Willian Borges da Silva raia wa Brazil amewaomba mabosi wake wampe ruhusa ya kusepa ndani ya London ili kuifuata familia yake nchini Brazil.

Winga huyo mwenye miaka 31 amesema kuwa kwa sasa ameikumbuka familia yake kwani hali ya kuwa mpweke muda mrefu imemchosha jambo linalomfanya aikumbuke familia yake.

Ligi Kuu England kwa sasa imesimamishwa kwa muda na inatarajiwa kurejea Aprili 30 ambapo awali ilitarajiwa kurejea Aprili 3 kutokana na kusambaa kwa Virusi vya Corona.

Wakati Ligi Kuu England inasimamishwa, Chelsea Ilikuwa imecheza mechi 29 na kujikusanyia pointi 48 zilizoifanya iwe nafasi ya nne kwenye msimamo.


“Nimekaa mbali na familia kwa muda mrefu, mimi nipo London kwa sasa familia yangu ipo Brazil nahitaji kwenda kuiona na kuwa karibu nao hali ya upweke inaumiza,” amesema.

BALAA LA KAKOLANYA LIPO NAMNA HII UWANJANI DITRAM NCHIMBI: NINAFANYA MAZOEZI KULINDA KIWANGO CHANGU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply