Uncategorized
ISHU YA BEKI WA AZAM FC MORRIS KUJIUNGA NA SIMBA IPO NAMNA HII
UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa una mkataba mrefu na nyota wao Agrey Morris ambaye anakipiga ndani ya Azam FC.
Beki huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji.
Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria,amesema kuwa Azam FC walimuongezea mkataba beki huyo kutokana na ubora wake akiwa ndani ya uwanja.
“Morris ni mchezaji wa Azam FC na mkataba wake aliongeza wakati akiwa Hospitali baada ya kuumia kwenye timu ya Taifa ya Tanzania ila kuhusu kuibukia Simba hilo kwa sasa halipo, mashabiki wa Azam FC wasiwe na mashaka.
“Mchezaji mzuri anahusishwa kujiunga na timu kubwa kutokana na umuhimu wake hilo lipo wazi lakini ukweli ni kwamba hakuna mazungumzo yoyote ambayo tumeyafanya kwa sasa na Simba,” amesema.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.