Uncategorized

MTAMBO WA MABAO NDANI YA AZAM FC AINGIA KWENYE RADA ZA YANGA

admin March 23, 2020 7:04 am


IMEELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mpango wa kumrejesha kundini mshambuliaji wao wa zamani Obrey Chirwa anayekipiga ndani ya Azam FC.

Chirwa kwa sasa ni kinara wa kutupia ndani ya Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba akiwa amefunga mabao nane sawa na David Molinga wa Yanga.

Wakati wa usajili wa dirisha kubwa msimu huu, Chirwa alikoswakoswa na Yanga kutokana na Kocha wa wakati huo Mwinyi Zahera kugoma kumpokea kutokana na kile alichoeleza kuwa ni mchezaji anayependa fedha.


Yanga ikiwa imecheza mechi 27 ambazo ni sawa na dakika 2,430 imefunga mabao 31 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 78.
SIMBA SASA WAANZA KUMVUTIA KASI NYOTA ANAYEKIPIGA MALAYSIA NAMUNGO WABISHI KWELI, CHEKI WANAVYOKULA SAHANI MOJA NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply