TIMU ya Chelsea imekubali kumpa ruhusa nyota wake Willian Borges Da Silva kurejea kuiona familia yake.
Winga huyo raia wa Brazil aliomba ruhusa ya kurejea kwao ili kuiona familia yake wakati huu wa tatizo la Virusi vya Corona.
Chelsea iliyopo London imekubali kumpa ruhusa winga huyo akamuone mkewe na wanae ambao wapo Brazil.
Kwa sasa Ligi Kuu England imesimamishwa kwa muda na inatarajia kurejea Aprili 30 endapo hali ya maambukizi itapungua na kutulia.
Nyota huyo amedumu ndani ya Stamford Bridge kwa muda wa miaka saba na mkataba wake unameguka Juni huku hatma yake kubaki ndani ya klabu hiyo kwani Cheksea ilitaka kumpa kandarasi ya mwaka mmoja yeye alitaka apewe ya miaka miwili.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.