Uncategorized

HIVI NDIVYO NYOTA WA POLISI TANZANIA ANAVYOLINDA KIPAJI CHAKE WAKATI HUU WA MAPUMZIKO

admin March 29, 2020 9:21 am


Marcel Kaheza, mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa kwa muda huu wa mapumziko ya Ligi Kuu Bara anafanya mazoezi binafsi ili kulinda kipaji chake.

Kaheza ametupia mabao saba na kutoa pasi tano za mabao amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ndani ya kikosi hicho akiwa ni kinara wa kutupia mabao.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa amekuwa akifanya mazoezi ili kulinda kipaji chake pamoja na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.

“Ninaendelea kulinda kipaji changu na kufanya mazoezi ili kuwa bora kwani mchezaji lazima afanye mazoezi ili kuzidi kujiimarisha.

“Pia ninachukua tahadhari ya Virusi vya Corona ili kulinda afya yangu pamoja na ndugu ambao wananizunguka,” amesema.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 29 za Ligi Kuu Bara.
Marcel Kaheza anayekipiga Polisi Tanzania amefunga mabao saba na ametoa pasi tano za mabao

SAINI YA JADON SANCHO DILI KUBWA KWA TIMU KUBWA, CHELSEA NA UNITED ZAMUWANIA BERNARD MORRISON AWAPA SOMO HILI WACHEZAJI WENZAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply