Uncategorized

MBELGIJI WA SIMBA HESABU ZAKE ZIPO NAMNA HII

admin April 3, 2020 9:14 am


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa bado kuna mambo hayajakamilika ndani ya Simba kutokana na malengo waliyojiwekea hivyo iwapo Ligi Kuu Bara itarejea wataendelea pale walipoishia.

Ligi Kuu Bara pamoja na ligi nyingine duniani zimesimamishwa ili kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.

Wakati ligi ikisimamishwa Simba ilikuwa nafasi ya kwanza na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28.

“Tuna malengo ambayo tumejiwekea ambapo ilikuwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

“Imani yetu ni kwamba bado tuna kazi ya kufanya hivyo mambo yakiwa sawa tutaendelea pale tulipoishia,” amesema.

KOCHA MANCHESTER UNITED AWATAKA WACHEZAJI KUWATUMIA WAKE ZAO KUFANYA MAZOEZI PACHA YA BOCCO NA KAGERE ILIANZA KUNOGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply