Uncategorized

UBINGWA WA LIVERPOOL MASHAKANI IWAPO MSIMU WA 2019/20 UTAFUTWA

admin April 3, 2020 6:14 pm


IWAPO msimu wa 2019/20 wa Ligi Kuu England ukifutwa, Liverpool inabidi isahau kutwaa ubingwa licha ya kwamba inaongoza ikiwa na pointi 82 kibindoni.

Mamlaka za soka barani Ulaya wameeleza kuwa Kuna uwezekano mkubwa wa msimu huu wa 2019/20 kufutwa ikiwa shughuli za soka hazitarejea hadi kufikia Juni mwaka huu.

Aleksandr Ceferin, Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) amesema kuwa kuna mambo yanaweza kutokea kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Sababu kubwa ya kusimamishwa Ligi ni kupisha na kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona. “Kuna mpango A,B n C ligi zinatarajiwa kurejea katikati ya Mei, ikishindikana hapo inamaanisha kuwa msimu utakuwa umefikia tamati na umepotea.


 “Kuna uwezekano mambo yakiharibika basi kuanza upya msimu ujao tunalifanyia kazi na tutatoa majibu baada ya kulizungumza na wakuu wa Vilabu,” amesema Ceferin.

ALICHOKISEMA AUSSEMS KUHUS JONAS MKUDE YANGA SASA KUFUATA JEMBE JINGINE LA KAZI AS VITA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply