Uncategorized

DAU LA BEKI ANAYEWINDWA NA SIMBA NI PASUA KICHWA

admin April 9, 2020 10:14 am

INAELEZWA kuwa dau la nyota wa Coastal Union, Bakari Nondo ni zaidi ya milion 90 kutokana na uwezo wake alionao ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa.

Nondo amekuwa akihusishwa kutua ndani ya Simba ambao inaelezwa kuwa dau lao ni milioni 85 zilizowekwa mezani.

Nyota huyo ambaye pia ni nahodha wa Coastal Union amekiongoza kikosi chake kwenye mechi 28 na kimefungwa mabao 19 kikiwa ni cha pili msimu huu kufungwa mabao machache ndani ya ligi huku nafasi ya kwanza ikiwa ni kwa Simba ambao wamefungwa mabao 15 kwenye mechi 28 za ligi.

Meneja wa nyota huyo, Mussa Kassa amesema kuwa hawezi kutaja dau la mchezaji wake kwani anaamini kuwa uwezo wake ndio utakaompa thamani uwanjani.

“Ni mchezaji mzuri kazi yake inaonekana ila dau lake siwezi kuliweka hadharani ni makubaliano na timu ambayo inamhitaji,” amesema.

METACHA AMPONGEZA KAGERE, ASEMA ALIMZIDI UJANJA LAKINI IKAWA BAHATI ROMA YANOGEWA NA HUDUMA YA SMALLIG YAITAKA SAINI YAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply