Uncategorized

MANARA: CORONA IMETIBUA DILI LA WAZUNGU KUJA BONGO

admin April 10, 2020 11:36 am


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Ugonjwa wa Covid-19 unaonezwa na Virusi vya Corona umetibua dili lake la kuwaleta nchini Wazungu wa Klabu ya Olympique Lyonnais ambao walikuwa wanakuja kwa ajili ya kuangalia vipaji. 

Manara amesema kwamba alipata dili na klabu hiyo baada ya kwenda nchini Ufaransa hivi karibuni na walikubali kuja Aprili 28, mwaka huu lakini virusi hivyo vimetibua kila kitu. 

“Nilikuwa nimekubaliana na watu kutoka nje ya nchi nilipokuwa Ufaransa ila kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona mambo yametibuka, ni suala la kuomba dua ili kila kitu kiwe sawa,” amesema.
Virusi hivyo vimekuwa tishio duniani kutokana na kusambaa kwake kwa kasi na Ufaransa ni moja ya nchi ambazo zina maambukizi mengi.

HIZI NDIZO TIMU ALIZOKIPIGA NYOTA MWENYE RASTA ANAYEWINDWA NA YANGA KIUNGO HUYU WA SIMBA PANGA LINAMHUSU MAZIMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply