Uncategorized

MTUPIA MABAO NAMBA MOJA NDANI YA YANGA KUSEPA MAZIMA

admin April 13, 2020 2:27 pm
 KLABU ya ES Setif inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria imeweka ofa mezani kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa Yanga, David Molinga ‘Falcao’.

Nyota huyo ambaye ni mpachika mabao namba moja ndani ya Yanga amekuwa hana nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.
Nyota huyo kwa sasa anafikiria kusepa ndani ya kikosi hicho kutokana na kukosa namba ya kudumu tofauti na zama za Mwinyi Zahera ambapo alikuwa na uhakika wa kutumia dakika 90 uwanjani.

 Kocha  Mkuu wa Yanga, Luc Eymael alisema kuwa kinachomshinda Molinga uwanjani ni kushindwa kutulia sehemu moja huku akisema kuwa ishu ya kuondoka ndani ya Yanga lipo chini ya viongozi.

“Miongoni mwa wachezaji wazuri lakini anashindwa kutulia sehemu moja muda mwingi anazungukazunguka, akipata nafasi atakuja kuwa vizuri iwapo kuna masuala ya mchezaji kuondoka hayo yanahusu utawala.
NONGA: MUHIMU KWA WACHEZAJI KUCHUKUA TAHADHARI NA KUFANYA MAZOEZI HAWA IHEFU WATOE DARASA KWA WAKONGWE NAMNA YA KUJIJENGA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply