Uncategorized

NONGA: MUHIMU KWA WACHEZAJI KUCHUKUA TAHADHARI NA KUFANYA MAZOEZI

admin April 13, 2020 1:57 pm

NAHODHA wa Lipuli, Paul Nonga amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuchuukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona huku wakilinda vipaji vyao kwa kufanya mazoezi binafsi.

Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji wamekuwa wakifanya mazoezi binafsi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa kwa sasa ni ngumu kufanya mazoezi kwa pamoja lakini kila mmoja anachukua tahadhari kujikinga na Corona na kulinda kipaji chake.

“Kwa sasa imekuwa ngumu kufanya mazoezi ya pamoja kwani hakuna ruhusa ya kufanya mijumuiko isiyo ya lazima, kikubwa ni kuona kwamba kila mmoja anachukua tahadhari.

“Kwa wachezaji pia ipo wazi kwamba ni lazima kufanya mazoezi ili kulinda vipaji na ni wakati ambao tunajipima wenyewe namna gani tunakuwa na nidhamu ya kufanya kile ambacho tunaelekezwa bila kusimamiwa,” amesema.

POLISI TANZANIA YATUMA UJUMBE HUU KUHUSU VIRUSI VYA CORONA MTUPIA MABAO NAMBA MOJA NDANI YA YANGA KUSEPA MAZIMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply