Uncategorized

MTIBWA SUGAR YAWATUMA WACHEZAJI KUWA MABALOZI KWA JAMII

admin April 14, 2020 7:57 am


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa umewatuma wachezaji wao wa Mtibwa Sugar kuwa mabalozi kwenye jamii kuhusu janga la Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema kuwa wamewambia wachezaji wao wawe makini na wahakikishe wanachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

“Tupo kwenye wakati mgumu kwa sasa ila imani yetu ni kwama hili litapita pia na maisha yataendelea, ila kikubwa ambacho tumewaambia wachezaji wetu wahakikishe wanakuwa mabalozi katika jamii katika kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

“Wachezaji wapo nyumbani na wameambiwa wawe makini katika kazi wanayofanya na wawe makini kwani Virusi vipo na vinaua hivyo wanapaswa wawe mabalozi katika hili bila kusahau dua,” amesema.

SIMBA: YANGA WAISHUKURU GSM BILA WAO KUTUFUNGA INGEKUWA NDOTO ALIYEWATUNGUA SIMBA NA YANGA AJICHIMBIA BUNDA KWA SASA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply