Uncategorized

RAMSEY AMPA TANO CR 7

admin April 14, 2020 5:57 am
SUPASTAA wa Juventus, Cristiano Ronaldo, amefagiliwa na mchezaji mwenzake, Aaron Ramsey kwa uanamichezo wake, ubora na kufuata maadili ya kazi yake.
Ronaldo alikuwa akifurahia msimu mwingine bomba baada ya kufunga mabao 25 katika mechi 32 kabla ya msimu kusimamishwa na Corona. Ramsey alitua Turin mwanzoni mwa msimu huu akitokea Arsenal lakini ameshaona vitu vya tofauti kwa Ronaldo.
“Ni mchezaji wa kipekee ni wa kwanza kwenda gym, anakuwa wa kwanza kwenye kila kitu. Ni mpambanaji, anataka kushinda kila mechi, akimaliza, anaanza kupiga mazoezi ya mipira ya faulo na mambo kama hayo.
“Huhitaji nikwambie jinsi alivyo mkali, ni mmoja wa wachezaji bora katika historia ya soka.
Ramsey alisema aliamua kwenda Juventus ili kutwaa makombe zaidi, likiwemo la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
VIFUAVIWILI:WATANIELEWA TU SIKU MOJA LICHA YA KUNIBEZA KWA SASA MABOSI WA YANGA WAPANIA KUWA NA KIKOSI MATATA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply