Uncategorized

SIMBA YA SENZO IKO ‘NEXT LEVEL’ AISEE …WACHEZAJI KUFANYA MAZOEZI KWA VIDEO CALL

admin April 15, 2020 6:00 pm

NI mwendo wa teknolojia tu sasa hivi, hili ndio linalofanyika kwenye taasisi mbalimbali kwa nchini kutokana na kuwepo ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Teknolojia sasa inaweza kuwa miongoni mwa vitu vinavyopunguza mikusanyiko ya watu ambayo imepigwa marufuku.

Katika kikosi cha Simba wachezaji wa timu hiyo wamepewa ratiba ya kufanya mazoezi nyumbani au mahala ambapo hakuna mikusanyiko ya watu ili kulinda viwango vyao na utimamua wa mwili kama ilivyokuwa hapo awali wakati Ligi Kuu Bara inaendelea.

Ofisa Mtendaji mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema wao mbali ya kuwapa wachezaji wao programu maalumu ya kwenda kufanyia mazoezi nyumbani kwao au mahala walipo huwa wanatumia simu kuwapigia (Video Call), ili kuwaona jinsi wanafanya
pamoja na maendeleo yao.

“Tumeamua kufanya hivi ili wachezaji wetu kuwa sawa kimwili na muda wote ambapo ligi ikirudi tukikutana kwa pamoja tuwe tayari kwa mashindano na si kuanza tena chini kujenga utimamu wa miili ya wachezaji wetu,” amesema Senzo.

BAADA YA SVEN KUONYESHA KUMUHITAJI..KIUNGO NAMUNGO AMEFUNGUKA HAYA..!! AZAM FC YAJITOSA KUWANIA KIFAA CHA CONGO KINACHOTAKIWA SIMBA NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply