Uncategorized

BERNARD MORRISON;MAMBO YANGEKUWA SAWA, NINGESAINI SIMBA

admin April 16, 2020 11:01 am


KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amesema kuwa kama mabosi wa Simba wangemalizana na meneja wake basi angesaini jumlajumla kwa watani hao wa jadi ila haikuwezekana.

Morrison alikuwa anawindwa na Simba ambao walikuwa wanahitaji huduma yake baada ya kugundua kwamba alisaini kandarasi ya miezi sita alipotua Bongo.

Kiungo huyo amesema:”Mchezaji mzuri anajulikana kutokana na kazi yake ndani ya uwanja, Simba walikwama kuzungumza na meneja wangu ambaye niliwaelekeza baada ya wao kuonyesha nia ya kunitaka.

“Labda kama wangekubaliana na meneja wangu huenda ningecheza Simba ila wao walishindwa kufika mwisho kwani hilo suala nililiacha mikononi mwa meneja wangu,” amesema.

Baada ya kutua Bongo mechi yake ya kwanza ilikuwa mbele ya Singida United na alitoa pasi yake ya kwanza ya bao lililofungwa na kiungo mwenzake, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda wakati Yanga ikishinda mabao 3-1.

KOCHA MKUU WA SIMBA ATOA NENO LAKE KWA MSHAMBULIAJI NAMBA MOJA BONGO MNATA ATAJA ANACHOKIPATA KUTOKA KWA SHIKALO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply