Uncategorized

CORONA YASABABISHA KUYUMBA KIDOGO KWA YANGA

admin April 19, 2020 3:29 pm

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa kipindi hiki kigumu cha Virusi vya Corona uendeshaji umekuwa na changamoto kubwa kutokana na mambo kuyumba kutokana na janga hili.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamisha na Serikali kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kuna mambo ambayo yameyumba kidogo kutokana na kubadilika kwa ratiba tofauti na awali ilivyokuwa.

“Kuna changamoto kidogo kwenye uendeshaji ukizingatia kwamba gharama bado zinaendelea na wachezaji wanahitaji stahiki zao hivyo kutokana na janga la Corona kuna myumbo kidogo.

“Ila yote kwa yote hii ni kwa sababu yale ambayo yalikuwa yanafanyika mwanzo kwa sasa yamebadilika hivyo ratiba zinakuwa tofauti jambo ambalo linasababisha kuyumba, hivyo maombi yetu hili lipite ili turudi katika ubora,” amesema.

MLINDA MLANGO WA SIMBA AMEMISI MAMBO MAKUBWA MATATU NDANI YA LIGI KUU BARA KUNA STRAIKA WA BURUNDI ANAITAKA YANGA, KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply