Uncategorized

HUYU NAYE KICHWANI ZIMO, UWANJANI ANA BALAA ANATAJWA KUTUA YANGA

admin April 19, 2020 9:29 pm
PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli, kichwani ana Stashahada ya Ulipuaji Miamba ambayo aliamua kujiongeza baada ya kumaliza kidato cha sita na aliipata kwenye Shirika la Elimu Mwanza.
Ametupia mabao 11 na pasi nne za mabao na Lipuli ipo nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi  29 na ina pointi 33 ikiwa imetupia mabao 35.
Nonga anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Kariakoo Yanga ambao wanahitaji kupata saini yake ya nyita huyo aliyewahi kuichezea timu hiyo na kuomba kusepa baada ya kukosa namba kikosi cha kwanza.

Kwa sasa amekuwa kwenye ubora wake na inaelezwa kuwa amewaambia mabosi wake Lipuli kwamba anahitaji kusepa ndani ya klabu hiyo ili apate changamoto mpya.
DODO YA ALIKIBA YAWEKA REKODI YA AJABU BONGO HIKI NDICHO WANACHOKIKOSA WANA SIMBA KWA SASA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply