Uncategorized

KOCHA STARS ATAJA SABABU YA MAKIPA KUWA NA VIWANGO VYA KUPWA NA KUJAA

admin April 19, 2020 2:29 pm

ETTIENE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa kinachowakwamisha makipa wengi kushindwa kuwa kwenye ubora wao ni kutokana na makocha ambao wanawafundisha.

Ndayiragije amesema kuwa kwa sasa kumekuwa na makocha ambao wanaamua kuwafundisha makipa ilihalli hawana uwezo mkubwa wa kuwafundisha makipa.

“Unajua kwa sasa mambo mengi yamebadilika, kuna wale ambao wanaamua kuwafundisha makipa ilihali hawana uwezo wa kuwa kwenye fani hiyo kisa walikuwa makipa zamani wakaacha jambo ambalo linawafanya wakutane muda mwingine na ugumu kwenye kuwafundisha.

“Pia kwa hapa Tanzania bado kuna changamoto hiyo ila kutokana na ushindani kidogo uliopo kuna mabadiliko kila siku yanatokea,” amesema.

Ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania miongoni mwa makipa ambao huwa wanagombania namba mbele ya Juma Kaseja ni Aishi Manula na Metacha Mnata.

HUYU NI YULE BEKI TEGEMEO WA GOR MAHIA SASA INAELEZWA SIMBA WANAISAKA SAINI YAKE HUYU NDIYE MCHEZAJI WA KWANZA KUFUTA MACHOZI YA KIPA WA LIVERPOOL

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply