Uncategorized

BALAA LA CHAMA WA UCHEBE NA SVEN LIPO HIVI UWANJANI

admin April 20, 2020 11:59 am

CLATOUS Chama kiungo mshambuliaji wa Simba amezidi kuwa imara mbele ya Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck kwa kutumia dakika nyingi uwanjani.

Kabla ya Sven kutua Bongo, Chama kwenye mechi 10 alizosimamia Kocha Mkuu, Patrick Aussems ambazo ni sawa na dakika 900 alitumia dakika 532.

Wakati Sven akiwa amesimamia mechi 18 mpaka sasa kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ametumia dakika 1,213 uwanjani.

Jumla Chama ndani ya Simba ambayo imecheza mechi 28 sawa na dakika 2,520 ametumia dakika 1,745 uwanjani akicheza jumla ya mechi 23.

Amefunga mabao mawili na kutoa pasi saba za mabao ambapo jumla amehusika kwenye mabao tisa ya Simba kati ya 63 ambayo yamefungwa mpaka sasa.

GIROUD AKUBALI KUTUA INTER MILAN MSIMU UJAO MSHAMBULIAJI HUYU WA BURUNDI AKUBALI KUVAA UZI WA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply